Swahili - Kiswahili

Mji wa Stirling hujivunia kuwa na mmojawapo wa jumuiya ya utamaduni-anuwai sana nchini Australia. Tunaahidi kutolea wakaazi wetu wasiosema Kiingereza na msaada wanaohitaji kupatia huduma zetu.

Msaada wa lugha na utafsiri

Msaada wa lugha ya Kiingereza

Ikiwa unahitaji msaada wa kuboresha ustadi wako wa lugha ya Kiingereza, unaweza kustahili msaada kutoka mradi wa serikali ya Australia wa Mpango wa Kiingereza kwa wahamiaji (AMEP).

Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya AMEP.

Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS)

Huduma za ukalimani na utafsiri zinapatikana kwa wakaazi wetu wasiosema Kiingereza kupitia Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS). Huduma inatolea utafsiri wa lugha kwa mawasiliano wa kusema na kuandikia katika lugha 160 kwa:

  • Mashirika ya Serikali
  • Mashirika yasiyo faida
  • Biashara.

Kutumia huduma hii, tafadhali wasiliana na TIS kwenye 131 450 na umwambie mwenye simu kwamba unataka kuwasiliana na Mji wa Stirling.

Idara ya Huduma za Jamii (DSS)

Idara ya Huduma za Jamii (DSS) inatolea huduma za utafsiri bila malipo kwa watu wanaoishi kwa kudumu nchini Australia, na kwa watu waliojiandikisha katika AMEP. Kwa habari zaidi, tafadhali piga simu DSS kwenye 1800 962 100.

Tafadhali kumbuka, ukitaka kuwasiliana na DSS na msaada wa mkalimani, tafadhali pigia simu Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS) kwenye 131 450 na umpe mwenye simu nambari ya simu ya DSS.

Huduma zetu

Mji wa Stirling unatoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Hizi ni pamoja na:

Takataka na urejelezaji

Mapipa ya makaazi

Mji wa Stirling unaendesha mfumo wa mapipa-matatu kwa:

  • Takataka ya kawaida
  • Urejelezaji
  • Takataka kijani.

Mapipa ya takataka ya kawaida yanakusanyika kila wiki. Mapipa ya kurejeleza na takataka ya bustani yanakusanyikwa kila wiki mbili kwa zamu.

Wakaazi wanashauriliwa kugawia vizuri takataka katika mapipa mbalimbali na msaada wa Mwongozo wa Takataka na Urejelezaji. Kuchagua takataka vizuri kunamaanisha kuepuka kutupa takataka kujaza ardhi tu na kupanga baadaye yenye kuendeleza kwa jamii yetu.

Zoni Bure za Wi-Fi

Wakaazi na wageni wanaweza kufurahisha kufika mahali pengi pa Wi-Fi ya bure katika maktaba, vituo vya mapumziko vya Mji na Kituo cha Utawala kwa Stirling.

Makataba ya Stirling

Mji wa Stirling una makataba sita ambayo yanatolea huduma mbalimbali kama vitabu na nyenzo, Wi-Fi ya bure, kompyta, huduma za kuchapisha, kupiga fotokopi na kukodisha chumba.

Ili kuwa mwanachama, tafadhli leta ID ya picha zilitolewa na serikali inazojulisha sahihi, pamoja na ushahidi ya anwani ya makaazi, kama bili ya matumizi.

Msaada na huduma za jamii

Mji wa Stirling hutolea huduma mbalimbali za msaada kwa familia, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.

Kukodi mapumziko na makutano

Mji wa Stirling una zaidi ya bustani na mibuga 400, vituo saba vya mapumziko, vituo vitatu vya kuogelea, na sehemu mbalimbali kubwa ya makutano panapopatikana kwa kukodisha.

Kupanga na kujenga

Timu ya huduma za maendeleo za Mji wa Stirling inatoa msaada na ushauri kuhusu maombi, majenzi na matumizi ya ardhi.

Wanyama na wanyama wapenzi

Wanyama na wanyama wapenzi wanakuwa na kazi nzuri katika ustawi wa jamii na wanaleta furaha na urafiki kwa wengi wao wa wakaazi wetu. Mji wa Stirling wanaangalia mahitaji ya wanyama, wanyama wapenzi na wamilikaji wenyewe wao, na mahitaji ya jumuiya mzima kupita siasa na huduma zetu.

Kuandikisha wanyama wapenzi

Wamilikaji wenyewe wa wanyama wapenzi wanapashwa kuandisha paka na mbwa wao na Mji wa Stirling kwa mpangilio wa mwaka, miaka-mitatu na maisha yake. Uandikishaji wa mwaka na miaka-mitatu unamaliza kila Oktoba 31 na lazima ifanye upya tena.

Matukio

Mji wa Stirling unaendesha matukio, warsha na mashughuli wakati wowote katika mwaka. Kujua kwamba kuna tukio katika mtaa wako, tafadhali, angalia kalenda yetu ya matukio.

Matukio