Mji wa Stirling hujivunia kuwa na mmojawapo wa jumuiya ya utamaduni-anuwai sana nchini Australia. Tunaahidi kutolea wakaazi wetu wasiosema Kiingereza na msaada wanaohitaji kupatia huduma zetu.
Msaada wa lugha na utafsiri
Msaada wa lugha ya Kiingereza
Ikiwa unahitaji msaada wa kuboresha ustadi wako wa lugha ya Kiingereza, unaweza kustahili msaada kutoka mradi wa serikali ya Australia wa Mpango wa Kiingereza kwa wahamiaji (AMEP).
Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya AMEP.
Huduma za ukalimani na utafsiri zinapatikana kwa wakaazi wetu wasiosema Kiingereza kupitia Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS). Huduma inatolea utafsiri wa lugha kwa mawasiliano wa kusema na kuandikia katika lugha 160 kwa:
- Mashirika ya Serikali
- Mashirika yasiyo faida
- Biashara.
Kutumia huduma hii, tafadhali wasiliana na TIS kwenye 131 450 na umwambie mwenye simu kwamba unataka kuwasiliana na Mji wa Stirling.
Idara ya Huduma za Jamii (DSS)
Idara ya Huduma za Jamii (DSS) inatolea huduma za utafsiri bila malipo kwa watu wanaoishi kwa kudumu nchini Australia, na kwa watu waliojiandikisha katika AMEP. Kwa habari zaidi, tafadhali piga simu DSS kwenye 1800 962 100.
Tafadhali kumbuka, ukitaka kuwasiliana na DSS na msaada wa mkalimani, tafadhali pigia simu Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS) kwenye 131 450 na umpe mwenye simu nambari ya simu ya DSS.
Huduma zetu
Mji wa Stirling unatoa huduma mbalimbali kwa jamii.
Hizi ni pamoja na: